MAYA WA BONGO MOVIE APATA KIGUGUMIZI NDOA YAKE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/maya-wa-bongo-movie-apata-kigugumizi.html
Mkongwe kwenye kilinge cha filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’.
MKONGWE kwenye kilinge cha filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’,
amepata kigugumizi cha ghafla kuzungumzia ndoa yake ambayo maandalizi
yake ya awali yaliwahi kufanyika.Akizungumza na mwandishi wetu baada ya
kuulizwa kuhusiana na ndoa hiyo iliyokuwa ifanyike mwaka juzi, Maya
alishindwa kuzungumzia jinsi ilivyoyeyuka na badala yake aling’atang’ata
maneno huku akidai haelewi ilipoyeyukia.
“Kuhusu ndoa mh! yaani sijui bwana nitazungumza nini kuhusu hilo
daah, sijui hata iliishiaga wapi,” alisema Maya ambaye alitaka kuolewa
na ‘mzee’ mmoja hivi ambaye alikuwa akimficha jina lake.