EVERTON YAANZA VYEMA EUROPA LEAGUE,
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/everton-yaanza-vyema-europa-league.html
KLABU
ya Everton ya England imeanza vyema michuano ya Europa League baada
ya kuichapa Wolfsburg ya Ujerumani manbao 4-1 Uwanja wa Goodison Park.
Kikosi
cha Roberto Martinez kilionyesha ni moto tangu mapema tu kwenye mchezo
huo, baada ya Ricardo Rodriguez kujifunga mapema tu
akijaribu kuokoa shuti la Steven Naismith kuipatia Everton bao la kuongoza.
Seamus
Coleman akafunga la pili karibu na mapumziko na Leighton Baines
aliyechangia mabai yote ya awali, akafunga la tatu kwa penalti baada ya
Aiden McGeady kuchezewa
faulo.Kevin
Mirallas akafunga bao la nne dakika za mwishoni kabla ya Rodriguez
kuwafungia wageni bao la kufutia machozi kwa mpira wa adhabu wa dakika
ya mwisho.
Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard,
Coleman/Osman dk90, Stones, Jagielka,
Baines, Barry, McCarthy, McGeady, Naismith/ Gibson dk82, Mirallas na Lukaku/Eto’o dk69.
Wolfsburg:
Benaglio, Jung, Knoche, Naldo, Rodriguez, Luiz Gustavo/Guilavogui
dk77, Malanda/Hunt dk46, De Bruyne, Arnold, Caligiuri/Bendtner dk60 na
Olic.
