La liga: Fc Barcelona waicharaza Granada magoli 6-0
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/la-liga-fc-barcelona-waicharaza-granada.html
MSHAMBULIAJI
Leonel Messi amefikisha mabao 401 leo Barcelona ikishinda 6-0 dhidi ya
Granada katika La Liga usiku huu Uwanja Camp Nou.
Messi
kwa kufunga mara mbili leo, sasa ana mabao 401 aliyoifungia Barca na
nchi yake, Argentina katika mechi 524 jumla alizocheza akiwa ana umri wa
miaka 27 tu. Bao lingine la Barca limefungwa na beki Ivan Rakitic.
Ushindi
huo unakuja wakati kikosi cha Luis Enrique kinaelekea kwenye mchezo wa
Ligi ya Mabingwa Jumanne mjini Paris dhidi ya PSG.