ARSENAL YAPONEA CHUPUCHUPU EMIRATES....OXLADE-CHAMBERLAIN AOKOA JAHAZI!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/arsenal-yaponea-chupuchupu.html
Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain (kushoto) alifunga goli la kusawazisha dhidi ya Tottenham
MASHABIKI wa Emirates walishangilia kwa
matarajio ya kushinda mechi ya watani wa jadi wa kaskazini mwa London
baina ya Arsenal na Tottenham, lakini wametoka sare ya 1-1.
Arsenal walitawala mchezo na kushambuli zaidi, lakini hawakuweza kupata magoli.
Tottenham walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 56 kupitia kwa Nacer Chadli, lakini Alex Oxlade-Chamberlain aliisawazishia Arsenal mnamo dakika ya 74.
Alex Oxlade-Chamberlain akishangilia goli lake
Kiungo wa Tottenham, Nacer Chadli akiifungia klabu yake bao la kuongoza dhidi ya Arsenal