KIMENUKA: BAADA YA MANENO MBOFOMBOFU...MLELA AMPA ZA USO NORA WA BONGO MUVI
Msanii wa filamu Bongo, Yusuph Mlela.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/kimenuka-baada-ya-maneno.html
Msanii wa filamu Bongo, Yusuph Mlela.
KUFUATIA madai ya hivi karibuni ya mkongwe wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ kuwa baadhi ya waigizaji hawana sifa za kuwa wacheza sinema zaidi ya kuuza sura, msanii Yusuph Mlela amempa dongo zito akisema licha ya umri kuwa mkubwa, pia ana matatizo flani yanayomsumbua.
“Nora naona siyo kosa lake kwani alishaugua yule, isitoshe ameshakuwa bibi hivyo nimemsamehe na sina tatizo naye kwani najua, lingekuwa jambo la maana kama angetufuata na kutushauri kama mkongwe lakini si kwa njia aliyofanya,” alisema Mlela.
Mkongwe wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ Hivi karibuni Nora aliwataja mastaa wenzake wa filamu akiwemo Mlela, Chuchu Hans, Steve Nyerere, Kajala na Batuli akisema hawawezi kazi zaidi ya kuuza sura
NAHAYA NDIO MANENO YA MKONGWE WA FILM NORA
Mlela kama ananiona mm bb kwenye game ndo anatakiwa
kuyafanyia kazi mawazo yangu,nakuongeza nakuahidi kuongeza bidii,lkn
mengine aliyoongea nikama anajiridhisha mwenyewe kwa kuutoa ukweli,mi
nina matatizo gan ktk kuongea ukweli,na kama watanzania wangeweza kutaja
pia wangetaja wengi zaid ya hao so mi niwasemea watanzania ambao
wanajiuliza hii sanaa mbona haikui badala yake inadidimia na kuporomoka
kwa nakujiongeazea sifa mbaya kwenye tasnia,so mi nimeamua kuongea
ukweli kama mkongwe ili watanzania waone kwamba ss wakongwe tunaona na
inatuuma kuona kuna watu ambao wapo tu kwa majina lkn ni mizigo.
