H.BABA KUMFUNZA MTOTO WAKE KEYBOARD ASEMA AKIANZA KUONGEA ATAMPELEKA STUDIO
Muimbaji Hamis Baba maarufu kama H.Baba amemnunulia vifaa vya muziki binti yake, Tanzanite na kuanza kumfunza kuvitumia. Pia amesema...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/hbaba-kumfunza-mtoto-wake-keyboard.html
Muimbaji
Hamis Baba maarufu kama H.Baba amemnunulia vifaa vya muziki binti yake,
Tanzanite na kuanza kumfunza kuvitumia. Pia amesema mwanae huyo akianza
tu kuongea atampeleka studio.
H.Baba amesema mwanae huyo ana kila dalili za kuja kuwa mwanamuziki kama wazazi wake.
“Mwanangu
mimi ana dalili zote za kuja kuwa mwanamuziki kwa sababu kila kitu
anakionyesha,” H.Baba ameiambia Bongo5. “Nimemnunulia keyboard lakini
nimemwachia ndani kaanza kubinya mwenyewe anajua nikibonyeza hapa inalia
hii na hii. Mimi nakuwa namwonyesha piga hapa piga hapa. Yaani namuomba
mwenyezi Mungu tu akiweza kuchanganya maneno tu basi anaingia kwenye
muziki moja kwa moja.”
