Ebola:Amri ya kutotoka nje yatekelezwa
Lengo la amri hii ni kuhakikisha kuwa kila mtu amekaa nyumbani huku wahudumu wa afya wakiendelea kuwatafuta wagonjwa kwa lengo ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/ebolaamri-ya-kutotoka-nje-yatekelezwa.html
Lengo la amri hii ni kuhakikisha kuwa kila mtu amekaa nyumbani huku
wahudumu wa afya wakiendelea kuwatafuta wagonjwa kwa lengo la kuwaweka
karantini ili kuzuia kuenea zaidi kwa Ebola.
Alhamisi, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilitangaza kuwa mlipuko huo ni tishio kwa usalama na amani duniani.
Baraza hilo liliomba mataifa yote kusadia katika harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Mvua kubwa iliyoshuhudiwa mjini Freetown hapo Alhamisi haikuwazuia
maelfu ya wananchi wa Sierra Leone kwenda sokoni na pia katika maduka ya
jumla kununua vyakula vya kutosha kabla ya amri ya kutotoka nje
iliyotangazwa na rais kuanza kutekelezwa.
Serikali ya Sierra Leone inaanimi hatua hii itasaidia pakubwa katika
harakati za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola ambao umeathiri wilaya
13 kati ya wilaya 14 zilizo nchini humo na kusababisha watu zaidi ya 500
kupoteza maisha yao.


