Baba mzazi apoteza maisha kwa kupigwa viboko na wanae.(mkoani Kagera)
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/baba-mzazi-apoteza-maisha-kwa-kupigwa.html
Jeshi la Polis mkoani Kagera linawashikilia watoto watatu,kwa tuhuma za kumpiga fimbo baba yao mzazi na kumsababishia kifo.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polis mkoani hapa Gilles Muroto,alisema tukio hilo
lilitokea mnamo mwezi Septemba 15,katika kijiji cha Mkunyu kata Kikukuru
tarafa Mabira wilayani Kyerwa,ambapo watuhumiwa hao ambao hawakutajwa
majina yao kutokana na umri wao kuwa chini ya miaka 18,walimuua baba yao
mzazi Henry Siliakus(62)kwa kumchapa fimbo hadi akapoteza uhai wake.
Muroto
alisema watoto hao ambao kati yao mmoja mwenye umri wa miaka 17
anasoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Mkunyu,huku mwenye
umri wa miaka 13 ni mwanafunzi wa darasa la nne na mwenye umri wa miaka
11 ni mwanafunzi wa darasa la tatu, wote wakiwa wanasoma katika shule za
msingi Mkunyu.
Alisema
mzazi huyo alikumbwa na mauti hayo kutokana na kupigwa fimbo nyingi
kichwani akiwa nyumbani kwake,huku sababu ya awali ya mtafaruku huo
uliosababisha kifo ikidaiwa kuwa ni ugomvi wa baba na watoto wake,kwa
kile kilichodaiwa marehemu kuwa na tabia ya kuuza chakula cha familia na
kuwaacha watoto wakitaabika.
Hata
hivyo,alisema jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya
tukio hilo na litawafikisha mahakamani watoto pale taratibu za kisheria
juu ya umri wao zitakapokamilika. ITV
