DIMPOZ, VANESSA MDEE WAKIFANYA YAO
SIKU chache baada ya mkali wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuripotiwa kuwa anatembea na mwanamitindo Jokate Mwegelo, imed...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/dimpoz-vanessa-mdee-wakifanya-yao.html
SIKU chache
baada ya mkali wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuripotiwa
kuwa anatembea na mwanamitindo Jokate Mwegelo, imedaiwa kuwa amemmwaga
na kuhamishia ‘mahaba niue’ kwa mtoto mzuri anayefanya muziki wa Bongo
Fleva, Vanessa Mdee.
Tukio
la kudhihirisha kwamba wawili hao ni wapendanao lilitokea juzikati
walipokuwa kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta katika Mikoa ya Iringa na
Morogoro ambako paparazi wetu aliwafuatilia hatua kwa hatua.
Chanzo
chetu kilicho karibu na wawili hao kilipigilia msumari wa uwepo wa
penzi motomoto kati ya wawili hao kwa kudai hata ukaribu wa msanii Jux
na Vanessa ulioripotiwa hivi karibuni katika vyombo vya habari, ulikuwa
ni upambe tu kwa Dimpoz.
“Jux alikuwa mpambe tu kwa Dimpoz wala hakuwa na uhusiano na Vanessa kama wengi walivyokuwa wakifikiri,” kilisema chanzo hicho.
Mara
baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha kibao zinazowaonesha wawili hao
wakipeana kampani ya karibu kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo,
alimvaa Dimpoz na kumuuliza kama ndiyo ameamua kujisevia moja kwa moja
au vipi, msikie alichojibu:
Wakikonga vyoyo za mashabiki.
“Ujue
kuna vitu unaweza kujitahidi sana kubishana na watu lakini kuna muda
inabidi uwe mpole tu kama hii ishu yangu na Vanessa maana walishaongea
sana juu ya uhusiano wetu, sasa nashindwa hata namna ya kumwepuka.
“Hatujawahi
kugombana hata siku moja na sina jinsi ya kuepuka kufanya naye chochote
maana kama ishu ya mapenzi kati yetu ipo wazi na hakuna jipya ambalo
naweza kusema watu wakanielewa,” alisema Ommy Dimpoz.Alipoulizwa Vanessa kuhusiana na uhusiano wao, aliishia kucheka tu na kudai hakuwa na cha kuzungumza.