BALOZI SEIF ALI IDD AKANUSHA MADAI MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA GAZETI LA MTANZANIA .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akikanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Jumat...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/balozi-seif-ali-idd-akanusha-madai.html
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akikanusha
taarifa zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba,
2014.
Waziri
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud
akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya
kukanusha taarifa zilizoandikwa na Gazeti hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakifutailia kwa makini taarifa toka Balozi Seif Ali Idd.
BALOZI
SEIF ALI IDD AKANUSHA MADAI MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA GAZETI LA
MTANZANIA KUHUSU KUJIUZULU KWA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd amekanusha madai
mbalimbali yaliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba,
2014 ambalo liliandika kuwa ‘Siri zavuja za AG Zanzibar kujiuzulu’.
Akikanush
taarifa hizo, Mhe. Balozi Idd amesema kuwa Mhe. Othman alitakiwa
ashiriki katika kamati kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa upande wa Zanzibar lakini kutokuwepo kwake katika Kamati
sio kikwazo cha kupatikana kwa Katiba, kwani waliokuwepo ndani ya kamati
kwa upande wa Zanzibar walitosheleza kuiwakilisha Zanzibar kikamilifu.
Mhe.
Balozi Idd alifafanua kuwa Mjumbe kuchaguliwa katika kamati na kukataa
kuhudhuria ni maamuzi yake binafsi na hakuna lazima ya mjumbe
kuchaguliwa kuingia katika kamati fulani ikawa ndiyo kifungo licha ya
kwamba atakuwa na wajibu wa kuendelea kufanya kazi katika kamati hiyo
hadi mwisho.
“Sisi
kama Serikali tunakanusha suala la sintofahamu iliyoandikwa na gazeti
hilo ambayo imedai kwamba Viongozi wa juu wa CCM walikutana kwa dharura
na kuazimia kumfukuzwa kazi kwa Mwanasheria huyo kwa kile walichodai
amekisaliti Chama”, alisema Balozi Idd.
Akizungumzia
juu ya uwepo wa hoja 17 ambazo zilitakiwa kuwasilishwa na Mwanasheria
Mkuu huyo, aisema kwamba Mwanasheria hiyo tayari alishaziwasilisha n
azote ziliingizwa katika Rasimu ya Katiba isipokuwa Hoja Nne ambazo bado
zinafanyiwa kazi.
Aidha
ameongeza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali hatakiwi kuwa muumini wa
Chama chochote cha siasa na ndiyo maana hata vikao vya chama hatakiwi
kuhudhuria, hivyo Mwanasheria huyo wa Serikali si mteule wa chama bali
ni mteule wa Mhe. Rais was Zanzibar na ndiyo mwenye maaumuzi ya
kumuondoa ama kutomuondoa.
Akizungumzia
kuhusu tuhuma za kufanyika kwa kikao cha Mawaziri wote wa SMZ
wakiongozwa na Dkt. Shein ili kuelezwa taarifa ya Mwanasheria huyo juu
ya masuala 17 aliyotaka yaingizwe katika Rasimu ya Katiba alikanusha
kuwa, suala hilo sio kweli kwani baadhi ya waandishi wa habari
hawafahamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina Mfumo wa Umoja wa
Kitaifa ambao umeundwa na CCM na CUF.
“Kama
inavyoeleweka CUF hawamo katika Bunge Maalum la Katiba, sasa itakuwaje
washiriki kuchangia masuala ambayo wao kama sehemu ya UKAWA
hawakubaliani na kuendelea kwa Bunge hilo?”, alihoji Balozi Idd.
Mhe.
Balozi Idd amevitaka Vyombo vya habari kuandika habari zenye ukweli na
amewataka kupuuzia uvumi unaoenea katika mitandao ya kijamii kuhusu
vitisho vitolewavyo na baadhi ya watu wenye nia ya kuwatisha baadhi ya
wajumbe wa bunge hilo kwani vyombo vya dola linafahamu juu ya uwepo wa
vitisho hivyo na inavifanyia kazi.