DIAMOND AMTOA MACHOZI MENINAH
YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkar...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/diamond-amtoa-machozi-meninah.html
YALE madai
kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta
Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya kutaka
kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo.
Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem.
Hivi
karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala
kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya
chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga
na Amani kwa dakika kumi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kikizungumza
kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai
kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac
Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond.
Chanzo
hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza
kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo
wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
Ilisemekana
kwamba baada ya Wema kuzinyaka habari hizo kuwa anataka kunyakuliwa
‘beibi’ wake mbaya zaidi wanataka kufunga ndoa, malkia huyo mkubwa wa
sinema Bongo aligeuka mbogo na kuanza kuweka mikakati ya kumteketeza
Meninah asiweze kufunga ndoa na Diamond.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kuna
madai kwamba Meninah aliposikia Wema anamsaka usiku na mchana ili
amshikishe adabu, msanii huyo alishtuka kwa kuwa anaujua vizuri ‘mziki’
wa staa huyo.
VIKAO VYA HARUSI VYAFANYWA
Taarifa
ziliendelea kudai kwamba, vikao vya harusi vya chinichini vinaendelea
kufanywa huku wahudhuriaji wakiwa ni mdogo wa Diamond ambaye pia ni
mwanamuziki, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darlin’ pamoja na baadhi ya
ndugu wa upande wa mama Diamond ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo
kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa.
POMBE NA STAREHE VYATAJWA
Sababu
kubwa inayosemekana Wema kutemwa kuolewa na Diamond ni kutokana na
kuendekeza pombe na starehe jambo ambalo Meninah yupo nalo kando na
kwamba hivi sasa amekuwa akitimba kwa mama Diamond bila wasiwasi huku
akizama jikoni kupika, kupakua na kufanya kazi ndogondogo za ndani ili
kuthibitisha kuwa yeye ni mama bora.
DIAMOND AMTOA MACHOZI
Baada
ya kunyaka madai hayo, Amani lilimsaka Meninah na kumhoji juu ya sakata
hilo la kutaka kuolewa na Diamond ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.
“Yaani
sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na
Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote,
nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala hazina
ukweli wowote.
“Mimi
na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye. Kwanza
naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi kuwa
naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe akisikia
hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye jambo
ambalo si la kweli.”
“Wema
namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu
Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya
filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na
sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.”
Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.TUJIKUMBUSHE
Kwa wiki kadhaa sasa, Meninah na Diamond wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
