Amber Rose ashambuliwa kwa picha alizosambaza, amejisahau ni mke wa mtu – Mashabiki (18+)
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/amber-rose-ashambuliwa-kwa-picha.html
Huwa
haichukui muda mashabiki kushambulia mastaa mbalimbali hasa wanapoona
kwamba wanavuka mipaka na kuharibu maadili au kuendeleza vitu ambavyo
vinawatafutia umaarufu kwa njia mbaya.
Mdau
mmoja mkubwa wa muziki duniani alipokuja Afrika aliwahi kuwaambia
Watangazaji wa Radio ni kiasi gani ambavyo mastaa wa dunia wamekua
wakilipwa pesa nyingi kupiga picha wakiwa watupu na kuzifanyia biashara
kwa kuziuza mamilioni ya pesa kwenye Majarida pamoja na vyombo vingine
vya habari.
Yani
biashara imegeukia huko na akamtolea mfano Rihanna ambae aliwahi kupiga
picha za namna hii na kulipwa mamilioni ya fedha za Kitanzania kwa
sababu tu ya picha zake 7 za utupu zilizotumiwa.
Katika
siku za karibuni taarifa kubwa ambazo zimetangazwa mpaka na vyombo
vikubwa vya habari duniani ni kuhusu tatizo la kuvujishwa kwa picha za
utupu za watu maarufu wakiwemo Waigizaji wa dunia kama Meagan Good na
Gabrielle Union ambae alikuwepo Tanzania siku kadhaa zilizopita.
Katika
siku za karibuni taarifa kubwa ambazo zimetangazwa mpaka na vyombo
vikubwa vya habari duniani ni kuhusu tatizo la kuvujishwa kwa picha za
utupu za watu maarufu wakiwemo Waigizaji wa dunia kama Meagan Good na
Gabrielle Union ambae alikuwepo Tanzania siku kadhaa zilizopita.
Mashabiki
mbalimbali na watumiaji wa mitandao wamemshambulia Amber Rose na kusema
kwa sasa mama huyu wa mtoto mmoja aliepata na rapper staa Wiz Khalifa
ameshakua kiumri na tayari ni mke wa mtu hivyo haya mambo awaachie wenye
ulimbukeni wa umaarufu na pesa za haraka zinazoambatana na kashfa.
Kibaya
zaidi kilichofanya wengi wamlaumu ni baada ya kujulikana kwamba picha
hizi alizisambaza kwa makusudi na sio kama kisingizio cha wengine kwamba
wamepoteza simu au kuibiwa.
