TAZAMA BUNGE LA KATIBA LAANZA BILA UKAWA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/tazama-bunge-la-katiba-laanza-bila-ukawa.html
Nchini
Tanzania leo Bunge Maalumu la Katiba linaendelea na vikao vyake mjini
Dodoma katika mchakato mzima wa kutafuta katiba mpya. Bunge hilo
linarejea vikao vyake baada ya kikao cha kwanza kuahirishwa kwa ajili ya
kupisha vikao vya bunge la bajeti.
Hata
hivyo kundi linalojiita Katiba ya Wananchi, au UKAWA kwa ufupi,
halihudhurii vikao vya sasa likisema mapendekezo ya wananchi
hayajumuishwi katika mchakato huo, hasa kupuuziwa kwa muundo wa serikali
tatu kama ulivyopendekezwa na Rasimu ya Katiba
