JAMES RODRIGUEZ AKUTANA CRISTIANO RONALDO KATIKA 'MATIZI' YA REAL MADRID
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/james-rodriguez-akutana-cristiano.html
Wamekutana: Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakitoa dole kuashiria mambo 'supa' wakati wa mazoezi ya Real Madrid.
MWANASOKA
BORA wa dunia, Cristiano Ronaldo amekutana na kijana mpya wa Real
Madrid James Rodriguez katika mazoezi ya klabu hiyo mjini Madrid nchini
Hispania.Rodriguez alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya kutokea klabu ya
Monaco kwa dau la paundi milioni 60 baada ya kuonesha kiwango kikubwa
katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu na kutwaa
kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa mashindano.
Ronaldo akifanya mazoezi katika uwanja wa Valdebebas
Ona
kitu hicho: Nyota wa Real (kutoka kushoto) Ronaldo, Karim Benzema,
Rodriguez na Raphael Varane wakati wa mazoezi ya Real Madrid
