MWANA MAMA MKAZI MWANZA AJIFUNGUA WATOTO WANNE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/mwana-mama-mkazi-mwanza-ajifungua.html
Watoto wa
Tecra waliozaliwa wakiwa ni wanne huku mmojawapo ambaye hakufunuliwa
uso akiwa amefariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa-Picha na Antony
Sollo-Malunde1 blog-Mwanza.
Muuguzi
wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Proscovia Leopod akimhudumia bi Tecra
baada ya kujifungua Picha na Antony Sollo-Malunde1 blog-Mwanza
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Tecra Kazimili(24) mkazi wa Lubili katika
wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza amjefungua watoto (4) kwa wakati mmoja
huku mtoto mmoja wa kiume akifariki muda mfupi baada ya mama huyo
kujifungua.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo si la
kawaida mama Tecra alisema hii ni mara yake ya nne kujifungua lakini ni
mara yake ya kwanza kujifungua watoto wanne kwa wakati mmoja.
Tecra
ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi katika Hospitari ya wilaya ya
misungwi Mkoani Mwanza alisema anamshukuru Mungu kwa kumjalia Afya njema
na kumuwezesha kujifungua watoto (4) pamoja na kwamba mmoja wa watoto
hao amepoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa.
“yote ni mipango ya mungu.”alisema Tecra
Tecra
aliongeza kuwa hiyo ni uzao wake wa nne lakini hana mtoto hata mmoja
kutokana na watoto wake wote (3) kufariki wanapofikisha mwaka moja hadi
mwaka mmoja na nusu kitendo kilichosababisha kufukuzwa na mume wake
Mussa Masalu aliyekuwa anaishi naye baada ya kuona watoto wanafariki na
kudaiwa kuwaua yeye mwenyewe jambo ambalo halina ukweli,alisema Tecra.
Pamoja na
hayo Tecra anawaomba Watanzania wasamalia wema watakaoguswa wamsaidie
kwa kuwa huyu aliyempa mimba hiyo si mumewe hivyo hana msaada wowote
atakaopata wakati atakapokuwa anaendelea kuwalea watoto wake hao.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Marco Mwita aliwaambia waandishi
wa Habari kuwa tukio hili ni si la kawaida kutokea mara nyingi wakina
mama wamekuwa wakijifungua watoto watatu na si wanne kama ilivyotokea
kwa Tecra.
Wauguzi
wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi wameonyesha utendaji uliotukuka kwa
namna ya kipekee jinsi waandishi walivyofika na kushuhudia namna
walivyokuwa wakimhudumia Tecra ambapo mmoja wa wauguzi hao Proscovia
Leopod 36 alikutwa akitoa huduma kwa upendo wa aina yake kwa kumsaidia
Tecra mambo mbalimbali aliyopaswa kuyafahamu ili kuhakikisha watoto hao
wanakaa salama.
Akifafanua
Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Proscovia Leopod alibainisha
baadhi ya mambo aliyokuwa akimfundisha Tecra kuwa ni namna ya
kuwanyonyesha watoto,kuwahudumia na kuwafunika shuka,na kumshauri ale
chakula cha kutosha na bora ili aweze kupata maziwa mengi kwa ajili ya
kuwanyonyesha watoto wake.
Pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu,wauguzi wa Hospitali hiyo wamesema kuwa,
“Tumefurahishwa
na jinsi Mungu alivyotujalia moyo wa kujituma kufuatana na mazingira
magumu ya utendaji wa kazi zetu,jambo hili siyo la mchezo tumehangaika
na kutumia uwezo wetu wote tulio nao kuhakikisha Tecra anajifungua
salama,tunaahidi kwa,tutamsaidia mama huyu kwa hali na mali mpaka hapo
hali yake itakapotengemaa na kuruhusu arudi kwao.” Walisema wauguzi hao.
Bi Tecra hana msaada,na kama unaguswa basi piga simu namba 0768102438
Na Valence Robert
