Flatnews

Malima akata makali posho za wajumbe watoro bungeni


Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima 
Hatua hiyo, imeelezwa pia na mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta wakati akitoa matangazo kuwa wajumbe wasiohudhuria vikao, hawatalipwa posho zao.


Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima amesema kuna baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba walioko nje, wamekuwa wakijipitisha “pembezoni mwa ukuta wa Bunge na wengine kupiga mluzi kutaka marafiki zao wawaandike majina” ili wapate posho.
Malima alisema juzi kuwa “wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, watapata posho zao watakapojiandikisha na kukaa bungeni, lakini si kwa mtu kupita pembeni mwa ukuta au kupiga muluzi ili aandikwe, hapo hatutatoa posho.
“Fedha za kila mjumbe zipo, kila atakayehudhuria kikao ndani ya Bunge atapata fedha stahiki, lakini hatuwezi kutoa fedha kwa mtu yeyote asiyehudhuria mkutano wala kujiandikisha...ninajua wapo watu wanapitapita pembeni huko, waje humu ndani.”
Hatua hiyo, imeelezwa pia na mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta wakati akitoa matangazo kuwa wajumbe wasiohudhuria vikao, hawatalipwa posho zao.
Sitta alisema kuwa kanuni zimeongezwa nguvu kwa wajumbe hasa katika suala posho na hazitapatikana kwa yeyote asiyehudhuria vikao vya Bunge.
Katika kikao cha juzi, wajumbe wengi walitaka wenzao ambao hawahudhurii vikao wachukuloiwe hatua na mwenyekiti na pia wanyimwe posho zao.

Post a Comment

emo-but-icon

item