Ebola yatikisa mfumo wa afya Liberia
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/ebola-yatikisa-mfumo-wa-afya-liberia.html
Waziri wa Habari wa Liberia
Lewis Brown ameiambia BBC kwamba mfumo wa afya wa nchi hiyo umeyumbishwa
na athari zilizotokana na mlipuko huo wa ugonjwa wa Ebola.
Kikosi cha jeshi nchini humo kimetawanywa kuweza
kuwazuia watu wasisafiri kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo, kutoka
katika maeneo ya vijiji yaliyokumbwa na ugonjwa huo.Wakati huohuo katika nchi jirani ya Sierra Leone, ambayo maeneo yote yamewekwa vizuizi kujaribu kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo. Waziri wa Habari wa nchi hiyo Alpha Kanu amesema inakatisha tamaa kuona kwamba dawa ambazo bado ziko katika majaribio, hazijasambwazwa nchini himo.
