MAN CITY WAMTAKA SERGIO AGUERO KAUNGUKA MITANO KABLA YA KUANZA LIGI KUU ENGLAND
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/man-city-wamtaka-sergio-aguero-kaunguka.html
Manchester City wanamtaka Sergio Aguero asaini mkataba mpya kabla ya kuanza msimu mpya.
MANCHESTER
City wanatumaini kuwa Sergio Aguero atasaini mkataba mpya utakaomfanya
alipwe paundi laki mbili na elfu 10 kwa wiki kabla ya kuanza kwa msimu
mpya.
Mabingwa
hao wa England wameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa Argentina yupo
katika mipango yao ya baadaye pamoja na nahodha Vincent Kompayn na
mazungumzo yanaendelea vizuri.
Barcelona
na Real Madrid wameweka wazi siri ya kuvutiwa na mshambuliaji huyo
mwenye miaka 26, lakini City wanafanya haraka ili kumuongezea mkataba wa
miaka mitano.
Mkataba wa sasa wa Aguero unamalizika
mwaka 2017, lakini Man City wanaona ni miaka michache imesalia, hivyo
kuna haja ya kumuongezea tena.
Aguero alikuwa anasumbuliwa na majeruhi msimu uliopita, lakini alifunga mabao 28 katika mechi 34 alizocheza.
City wameshaanza mazungumzo ya awali na
Kompany ili apewe mkataba wa miaka mitano na wanatumaini Edin Dzeko, Joe
Hart na James Milner watafuatia.
Milner mwenye miaka 28, anataka kuona ni mechi ngapi atacheza kabla ya kuongeza mkataba, lakini ni mchezaji muhimu kwa City.
Anasubiri mechi: James Milner yupo
makini kuangalia ni mechi ngapi atacheza kabla ya kuongeza mkataba na
kujifunga Manchester City.
