Flatnews

AZAM FC VS MTIBWA SUGAR HAPATOSHI TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI TAIFA DAR


KIKOSI cha pili cha mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc kitakabiliana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini , uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hii itakuwa mechi nzuri kwa timu zote kuangalia uwezo wa wachezaji waliowasajili na wale waliopandishwa kutoka timu za vijana.
Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga alisema wanauchukulia mchezo huo kwa uzito wa hali ya juu kwasababu ni nafasi nzuri kwa wachezaji wao kuonesha uwezo mbele ya timu bora ya Mtibwa Sugar.
“Ni kweli tutakuwa na mechi na Mtibwa Sugar. Hii ni timu nzuri yenye uzoefu mkubwa, hivyo naamini mchezo utakuwa ni mzuri. Tumejiandaa vya kutosha na tupo tayari kwa ajili ya mechi hiyo”. Alisema Jafar.
Pia Jafar alisema baada ya mechi hiyo, wachezaji wote watasafiri kuelekea nchini Rwanda ambapo Azam fc inashiriki michuano ya kombe la Kagame inayoanza kutimua vumbi leo Agosti 8.
Aliongeza kuwa vikosi vyote vya  Azam, A na B, vitakuwa mjini Kigali kwa ajili ya kombe la Kagame na ligi kuu. Kikosi cha wachezaji 20 tayari kipo Kigali na leo hii jioni kinaanza kampeni ya Kagame dhidi ya wenyeji Rayon Sport ya Rwanda.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar wao wamesema wamejiandaa vizuri na watatumia fursa ya leo kuonesha wachezaji wapya waliowasijili kwa ajili ya msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mecky Mexime amesema Azam ni timu bora, hivyo watapata changamoto nzuri ya kupambana nao.
 
“Tupo salama kabisa kwa ajili ya mchezo wa kesho. Safari hii tumechukua wachezaji kutoka ligi daraja la kwanza na michuano ya ligi kuu, hivyo watanzania waje kuwaona.” Alisema Mexime.
“Nawaheshimu Azam fc, ni timu nzuri, lakini Mtibwa ni wazuri pia. Kwahiyo tutaonesha mchezo mzuri.”
Mbali na mechi hii kubwa, mechi nyingine kwa upande wa soka zitakuwa  ni wabunge mashabiki wa Simba na wale wenzao wa Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na wengine wengi.
Pia kutakuwa na mapambo ya ngumi ambapo mapambano ya kawaida ni baina ya msanii wa Bongo Movie, Jacob Steven (JB) na Cloud 112, Said Memba na Khalid Chokaraa, lakini funga kazi ni baina ya Mada Maugo na Thomas Mashali.
Burudani mbalimbali za muziki kutoka kwa wasanii wa bongo Fleva akiwem Ali Kiba, Shilole na wengine zitakuwepo.
 
CHANZO NI MPENJA BLOG

Post a Comment

emo-but-icon

item