Flatnews

WASOMI WAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUJIENDELEZA


WASOMI wa vyuo vikuu nchini wamekumbushwa umuhimu wa kujiendeleza zaidi kielimu badala ya kuridhika na viwango vya elimu walivyonavyo ,sanjari na kutambua kuwa hivi sasa ajira hazipo bali kikubwa zaidi na muhimu kwao ni kujiajiri.

Rai hiyo imetolewa jana na Katibu mkuu wa mkoa wa vyuo vikuu vya Chama cha Mapinduzi, Christopher Ngubiagai, alipokuwa  akitunuku vyeti kwa viongozi waliomaliza muda wao miaka mitatu kutoka vyuo vikuu vya Arusha na Tumaini (Makumira) kwenye mahafali ya wanachuo hao wa mwaka wa tatu hafla iliyofanyika chuo kikuu cha Arusha.
Aliwaambia wahitimu hao wa mwaka wa tatu katika vyuo hivyo kuwa wasiridhike na kiwango cha elimu waliyoipata bali waongeze bidii kwa kuwa vyuoni ni mwanzo tu wakupata mafanikio katika maisha.wajiendeleze zaidi ili kuhimili soko la ushindani la kielimu katika nchi za Afrika mashariki na mataifa mengine Ulimwenguni.
Ngubiagai, ambae pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi,(NEC) alisema kuwa  kipindi kilichopo sasa ni kwa wasomi hao kutambua kuwa ajira kwa sasa hazipo na zinazopatikana hazitoshelezi mahitaji hivyo  ni lazima wajiandalie mazingira ya kujiajiri na si vinginevyo.
Alisema ni bora wasomi wakalitambua hilo mapema wataweza kuondokana na mawazo na fikra za kuajiriwa ambazo hazipo bali fursa iliyopo ni kujiajiri na wasisome kwa matarajio ya kuajiriwa ndani ya serekali au sekta binafsi.

‘’Ndugu zangu ninataka niwaeleze ukweli kwamba ajira zinazopatikana hazitoshelezi hivyo kikubwa ni ninyi wasomi wa vyuo vikuu  kusoma Kwa kujijengea mazingira ya kujiajiri na mafanikio yatapatikama.’’alisema ngubiagai.
 Na kamwe  wala wasitarajie kupata ajira kwa urahisi kutokana na ongezeko la wasomi wanaohitimu vyuo vikuu kila mwaka hapa nchini.

Aliwaambia wanavyuo hao kuwa Chama cha mapinduzi kimerejesha matawi  ya Chama kwenye vyuo vikuu ili kufundisha, itikadi ,malengo, ilani, Katiba ya CCM,elimu ya kujitegemea na uzalendo .

Ngubiagai, aliwaambia wasomi hao kuwa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi katika kurejesha matawi hayo  imepitisha kanuni  ambapo kutakuwa na katibu mtendaji wa  mkoa wa vyuo vikuu,wajumbe4 watano wa NEC, na wasomi watatu ,ambao wote watakuwa ni wajumbe wa NEC.

Kuhusu mikopo inayotolewa na bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Ngubiagai, amewaambia kuwa haitoshelezi kutokana na ongezeko la vyuo vikuu nchini hivyo wasomi hawana budi kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi ili mikopo iweze kutosheleza mahitaji.

Akifafanua tuhuma zinazotolewa na vyama vya kisiasa kuhusu ziara ya Katibu mkuu wa CCM, Komredi, Abdulahaman Kinana, kuandamana na mawqaziri , watendaji wa serikali na halmashauri kwenye ziara zinazofanywa na katibu mkuu huyo.

Ngubiagai, alisema kuwa Kinana ndie katibu mkuu wa CCM, anakagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi iliyoiweka na serikali ya CCM, madarakani, Ilani ambao ni mkataba kati ya wananchi na serikali yao.

Pia ziara hiyo inapokea na kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi ndio maana Katibu mkuu huyo anaambatana na mawaziri, au watendaji wa serikali na halmashauri ili kufafanua kero na kutoa majawabu sahihi .

Awali mwenyekiti wa tawi la chuo kikuu cha Arusha, Daniel Limbu, alisema kuwa  tawi hilo lilianza mwaka 2007 likiwa na wanachama 50 ,kutokana na chamgamoto zilizxojitokeza kipindi kilichopita, hivi sasa tawi lina wanachama zaidi ya 250 amao wote ni wanavyuo vikuu vya Arusha na  Tumaini.

Alisema kuwa katika mahafali hayo  wanachama 80 kutoka katika vyuo hivyo wamehitimu masomo yao vyuoni hapo,

Aliongeza kuwa vyuo hivyo pia vimepokea wanachama wapya zaidi ya 50 ambao ni wanavyuo mbali mbali hapa mkoani.

Post a Comment

emo-but-icon

item