WANANCHI NISAIDIENI MWENZENU
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/wananchi-nisaidieni-mwenzenu.html
Ndugu
Peter Mashiku anahitaji msaada wa matibabu ya haraka baada ya kuvimba
mkono wa kushoto kwa muda mrefu kutokana na pete alizokuwa amejaa
Ndugu
Peter Mashiku mkazi wa Mwatulole mjini hapa anahitaji msaada wa
matibabu ya haraka baada ya kuvimba mkono wa kushoto kwa muda mrefu,
sasa (kama anavyoonekana pichani)
Wakiongea na gazeti hili, wakaazi wa
maeneo hayo walisema chanzo cha tatizo hilo ni bwana huyo kuvaa pete
zaidi ya tatu kama sehemu ya urembo, jirani mmoja wa karibu ambaye
hakutaka jina liandikwe gazetini
“Tunashangaa hata sisi kwani
kufuatana na ucheshi, ukarimu na kulea familia kwanza tulichukua kama
mzaha kuona mwenzetu anavaa pete nyingi, baada ya wiki mkono ulianza
kuvimba sehemu za vidole “Alisema jirani huyo.
Madaktari wa hospitali ya wilaya hii
walisema kwa hatua aliyofikia anahitai msaada mkubwa kifedha ili apate
vipimo vya juu katika hospitali kubwa. Waliongeza kuwa pete hizo hivi
sasa zinaanza kumuathiri kwa kukata sehemu kadhaa na kama jitihada za
makusudi hazitachukuliwa na wasamalia wema huenda hali ikawa mbaya
zaidi.
Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya
msongo wa mawazo (saikolojia) Hellen Eric alisema mtu huyo anaonekana
kama ana wazimu, lakini vipimo vinaonyesha hali hiyo inatokana na wingi
wa vitu anavyofikiria kuhusu maisha yake.
“Akisaidiwa atarudia hali yake kama mwanzo kwani sio kichaa”
“Akisaidiwa atarudia hali yake kama mwanzo kwani sio kichaa”
Kwa hivyo kutokana na familia yake kusambaratika na wengine kuwa na hali duni anayetaka kumsaidia mawasilianao 0765 866264
