LANGA ATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU AFARIKI DUNIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/langa-atimiza-mwaka-mmoja-tangu-afariki.html
Tarehe kama ya leo mwaka jana,msanii wa Hip Hop, Langa Lileo, rais wa gheto mida ya jioni alitangazwa kuwa amefariki dunia,
kwa mujibu wa ripoti ya hospitali msanii huyo alikuwa anasumbuliwa na malaria kali, alilazwa siku moja katika hospitali ya taifa Muhimbili siku ya pili yake ndiyo akafariki. Safari ya Langa kimuziki ilianzia kwenye shindano la kusaka vipaji la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004, na wakapatikana washindi watatu wakaunda kundi la Wakilisha alikuwemo Langa, Shaa, na Witness, na ngoma yao ya Hoi.
Langa alizaliwa Desemba 22, 1985 Jijini Dar Es Salaam alisoma katika shule ya msingi Olympio na sekondari ya Loyola, pia alisoma Kampala Uganda, baadaye akapata Stashahada ya masoko katika chuo cha CBE,mkoani Dodoma.
You might also like:
