Flatnews

Wambura awatolea nje Friends of Simba


  • Kauli hiyo ya Wambura ni kama inalilenga moja kwa moja kundi la Friends of Simba linaloundwa na matajiri ambao wamekuwa wafadhili wa klabu hiyo kwa muda mrefu sasa.Share
MGOMBEA urais wa Simba, Michael Wambura, ametoa msimamo wake juu ya wafadhili wa klabu hiyo kuwa hawatapata nafasi katika uongozi wake kutokana na kuijengea klabu hiyo utegemezi na kushindwa kuikomboa.
Kauli hiyo ya Wambura ni kama inalilenga moja kwa moja kundi la Friends of Simba linaloundwa na matajiri ambao wamekuwa wafadhili wa klabu hiyo kwa muda mrefu sasa.
Awali Wambura alienguliwa katika mchakato huo wa uchaguzi utakaofanyika Juni 29 kabla ya kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kurejeshwa aliposhinda rufaa hiyo.
Wambura alienguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na baadhi ya wanachama kwa madai alisimamishwa uanachama mwaka 2010 baada ya kupeleka masuala ya soka mahakamani kitendo ambacho ni kinyume na taratibu za soka.
Akizungumza katika makao makuu ya Simba jana Alhamisi, Wambura alisema: “Wafadhili hawabanwi na sheria, wanafanya kwa wakati wanaojisikia hivyo ni ngumu kuendesha timu kwa njia hii. Pia ni ngumu kuendesha timu kwa kutegemea kitu kimoja kwa sababu klabu ni taasisi,  hivyo lazima iwe na wadhamini wanaotoa udhamini wao kwa makubaliano ya mkataba.”
Kwa upande mwingine, Katibu huyo wa zamani wa Simba, alisema kitendo kilichofanywa na klabu hiyo katika uongozi uliopita cha kuuza wachezaji tegemeo tena kwa mkopo katikati ya msimu, ni cha kushangaza kutokana na uwezo wa wachezaji wenyewe.
Simba iliwauza Emmanuel Okwi na Shomari Kapombe mwaka jana bila kuambulia hata senti tano ikisubiri malipo hayo kufanywa sasa.
“Huwezi kuuza wachezaji wakati ligi inaendelea, ni sawa na kuuza silaha wakati uko vitani, kamwe huwezi kushinda kwa njia hii. Nawashangaa sana waliofanya hivyo, halafu sasa wanajitokeza na kusema tunataka kulipwa na huyu mara hatutaki kulipwa na yule,” alisema Wambura.

Post a Comment

emo-but-icon

item