TFF YAINGILIA KATI KUOKOA MASHINDANO YA VIJANA UKANDA WA MAZIWA MAKUU.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/tff-yaingilia-kati-kuokoa-mashindano-ya.html
Na Bertha Mollel – Arusha.
Shirikisho
la kandada nchini Tanzania (TFF) limeingilia kati kuokoa mashindano ya
vijana ukanda wa maziwa makuu ambayo yalikuwa hatihati kufanyika na sasa
yataendeshwa kwa kushirikiana na waratibu wa mashindano hayo
Rollingstone Sports academy ya mjini Arusha chini ya mwamvuli wa mtandao
wa taasisi za za soka la vijana afrika mashariki na kati ECAYFA.
Mashindano
hayo ya wazi hufanyika kila mwaka mkoani Arusha mwaka huu yatafanyika
jijini dar es salaam na kushirikisha timu za vijana za under 20 na under
14 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, ,Zanzibar, na jamhuri ya
kidemokrasia ya kongo (DRC) na yatafanyika wiki ya kwanza ya mwezi
julay.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi wa rollingstone football academy
ally mtumwa masoud alisema mashindano hayo yalikuwa katika hatihati ya
kufanyika au kutofanyika baada ya TFF kuchelewa kutoa kibali cha
kuendesha mashindano hayo kwani taasisi hiyo iliandika barua ya kuomba
kibali tangu mwezi wa pili lakini hawakupatiwa kibali kwa wakati.
Mtumwa
alisema kuwa kufuatia kuchelewa kwa kibali hicho walishindwa kufanya
maandalizi ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta wafadhili na
kualika timu hususani zile zinazotoka nje ya nchi hali iliyosababisha
kufikiria kuyasogeza mbele au kutofanyika kabisa kwa mashindano hayo.
Hata
hivyo baada ya kufuatilia TFF walikiri kupokea barua hiyo na kusema
sababu zilizochangia kutofanyiwa kazi kwa barua hiyo ni piikapilika za
TFF kuhama ofisi kupisha ukarabati wa ofisi za karume lakini kwa kujua
umuhimu na ukubwa wa mashindano hayo waliamua yafanyike kwa ushiriano wa
pamoja na Rolly store kwa sharti la mashindano kufanyika jijini dare s
salaam ili waweze kushuhudia.
Hii
itakuwa mara ya pili kwa mashindano hayo ya 14 kufanyika nje ya Arusha
kwani mwaka 2012 yalifanyika nchini Burundi na utakuwa mwanzo wa
mashindano hayo kuzunguka katika mikoa na nchi mbalimbali ambazo
zitakuwa tayari kuandaa na kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuhudumia
malazi na chakula kwa timu zinazotoka nje ya nchi.
TFF,
rollingstone na ECAYFA wameunda kamati ya maadalizi itakayokuwa chini
ya uratibu wa afisa uhusiano na mawasiliano wa rollingstone Wilbrode
Alfonce na tayari nchi wanachama wa CAYFA na taasisi za sika nchini
Tanzania zimeshatumiwa barua za mialiko huku baadhi ya nchi kama burundi
,Kenya na DRC zikionyesha nia ya kushiriki.
