WAANAOTESA WATOTO SASA MOTO WAANZA KUWAWAKIA, SHUHUDIA HAPA
Jeshi la Polisi Changombe, Dar linamshikilia mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Neema na babu Ramadhan kwa RB namba CHA/RB/4645/20...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/waanaotesa-watoto-sasa-moto-waanza.html
Jeshi la Polisi Changombe, Dar linamshikilia mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Neema na babu Ramadhan kwa RB namba CHA/RB/4645/2014 UNYANYASAJI WA MTOTO wakidaiwa kumsulubu mjukuu wao (jina linahifadhiwa kimaadili).
Tukio la kuwatia nguvuni wahusika hao
lilijiri Mei 29, mwaka huu maeneo ya Buza jijini Dar, baada ya ya
majirani kusikia kilio cha mtoto huyo akiomba msaada ili kunusuru maisha
yake kutokana na kipigo kizito alichodaiwa kupewa na wawili hao.
Kwa mujibu wa majirani waliozingira
nyumbani hao, siyo mara ya kwanza kwa mtoto huyo ambaye ni yatima
kupigwa hivyo waliamua kuivamia nyumba hiyo kwa kuwataka wazee hao
waache kumpiga mtoto huyo jambo ambalo lilishindikana.
Majirani hao waliokerwa na kitendo
hicho walitishia kuchoma moto nyumba hiyo ndipo wazee hao wakaacha
kumpiga mtoto huyo na kutoka nje wakijitetea kuwa walikuwa wakimpiga kwa
kuwa alifanya kosa.
Walipohojiwa sababu za kumpiga mtoto huyo mara kwa mara, wazee hao walijitetea kuwa mtoto huyo ni mtukutu.
Majirani hao walidai kuwa siku za
nyuma wazee hao walishawahi kuandamana kuhusu unyanyasaji wa mtoto huyo
ambapo walishawahi kumripoti polisi Chang’ombe.
MAJIRANI WAANDAMANA
Ilielezwa kuwa majirani hao waliripoti
kuhusu unyanyasaji huo kwa Mjumbe na Afisa Mtendaji wa eneo hilo, Mary
Patrick ambaye alitoa taarifa kwa mwanaharakati wa kutetea haki za
watoto kutoka TUHIMIZANE, Cleophace Simioni ambaye alimchukua mtoto huyo
na kumpa huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka Ustawi wa Jamii kwa ajili
ya matunzo.
Waandishi wetu walifika nyumbani hapo
na kushuhudia mtoto huyo akiwa na majeraha ya kuchanwa mgongoni, makovu
ya moto na uvimbe usoni na kichwani.
Akizungumzia sakata hilo, mwanaharakati huyo alisema atapambana hadi hatua ya mwisho kutetea haki ya mtoto huyo.
Naye
Afisa Mtendaji wa Kata ya Buza, alisema kuwa anapinga vikali
unyanyasaji wa watoto katika eneo lake na kuapa kufuatilia kwa upande
wake ili kuhakikisha wanatoa mfano kwa watu hao.
Mwishowe wazee hao walifikishwa katika
kituo cha polisi Chang’ombe ambapo walifunguliwa shitaka hilo
wakisubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
