WAZIRI CHIKAWE AWAPA URAIA WA TANZANIA WAKIMBIZI WA KISOMALI 1,514 WA KAMBI YA CHOGO, HANDENI MKOANI TANGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/waziri-chikawe-awapa-uraia-wa-tanzania.html
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa cheti cha
uraia wa Tanzania, Mkimbizi wa Kisomali mwenye asili ya Kibantu,
Ramadhani Haji katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Chogo, Wilaya
ya Handeni mkoani Tanga. Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa
wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo ambao waliomba kupewa
uraia kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania.
Kulia kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole na Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya
wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu (hawapo pichani), baada ya
kutoa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika
Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake,
Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa
Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi
kwa amani. Kulia (Meza Kuu) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum
Chima. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke
na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia waliokaa),
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia), Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima (wapili kulia) na Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakimbizi wa
Kisomali wenye asili ya Kibantu baada ya kupewa vyeti vya uraia wa
Tanzania.Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514
waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika
hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia
halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze
kuishi kwa amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wakimbizi hao wakifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania



