MGONJWA WA SARATANI ALIYETELEKEZWA AFARIKI DUNIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mgonjwa-wa-saratani-aliyetelekezwa.html
Mgonjwa
wa saratani ambaye alidai kupewa tiba feki za mionzi katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road (OCRI), Pendo Shoo amefariki dunia juzi wilayani
Karatu akiwa safarini kuelekea Kirua Vunjo, Kilimanjaro kwa wazazi
wake.
Mdogo wa Pendo, Digna Shoo, alisema dada yake alifariki juzi, saa nne usiku wakati wanafamilia wakimfanya maombi.
“Alianza
kubadilika ghafla wakati tukiwa katikati ya maombi, alilegea na mgongo
wake ukawa kama unapinda hivi, tukamshika na tukamweka kitandani,”
alisema.
Digna
alisema kwamba baada ya kumweka kitandani mtumishi wa Mungu aliyekuwa
nyumbani hapo alimwombea na hazikupita dakika nyingi akakata roho.
Alisema Pendo alikwenda Karatu akitokea Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi
uliopita, kipindi ambacho hali yake ilikuwa imeshatetereka sana kiasi
cha kushindwa kutembea mpaka apate msaada wa mtu karibu.
