VIONGOZI WA MATAWI YANGA WAMTAKA MANJI KUWACHUKULIA HATUA KALI WANACHAMA WANAOCHOCHEA VURUGU
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/viongozi-wa-matawi-yanga-wamtaka-manji.html
Viongozi
wa Matawi ya Yanga wakiongozwa na Mohamed Msumi (wa kwanza kulia) . Picha na
Gervas Mwatebela
WAKATI
kwa ridhaa yao wanachama wa klabu ya Yanga waliamua kuuongezea muda wa mwaka
mmoja uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake, Yusuf Manji, huku baadhi
ya wanachama wa klabu hiyo wakitofautiana na maamuzi hayo, viongozi wa matawi wameutaka
uongozi kuwachukulia hatua wanachama na viongozi wa Matawi wanaochochea vurugu
katika klabu hiyo kwa mujibu wa katiba na miongozo ya klabu hiyo.
Wakizungumza
leo, viongozi hao wamewaonya baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakiongelea
masuala ya klabu hasa ya kiutawala pasipo kupata ruhusa ya mwenyekiti na
kuchafua hali ya hewa ndani ya klabu hiyo kuacha mara moja vinginevyo
watachukuliwa hatua kwani kanuni zipo wazi kwa sababu wanatakiwa kutoa maoni
yao kupitia mkutano mkuu na vikao halali ama kwa ruhusa ya mwenyekiti wa klabu
hiyo Yusufu Manji.
Baadhi
ya wanachama wamekuwa wakipinga maamuzi yaliyopitishwa na klabu hiyo katika
mkutano mkuu uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu wa kumuongezea mwaka mmoja
Yusufu Manji ili aweze kutekeleza malengo
aliyojiwekea
kitendo kinachodaiwa kwenda kinyume cha katiba ya klabu ya Yanga .