SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ILIVYOADHIMISHWA WILAYANI MKURANGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/siku-ya-mtoto-wa-afrika.html
Mgeni
rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid
akifuatilia sherehe hizo katika viwanja vya Shule ya Msingi
Kiparang’ada. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya
Kiparang’anda Mhe Karu Amani Karavina, na Kulia ni Mke wa Mbunge wa
Mkuranga,Mama Naima Malima.
Mke
wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akizungumza machache wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika,yaliyofanyika Juni 16 katika
shule ya msingi Kiparang'anda,wilayani Mkuranga.Kushoto ni Mgeni Rasmi
katika sherehe hizo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya
ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid
Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akikabidhi Sare na Vifaa vya shule kwa Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid kwa
niaba ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kiparang'anda,ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha siku Mtoto wa Afrika.
Picha ya Pamoja baada ya kukabidhiana vifaa mbali mbali.
Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid
akijaribu kusukuma Baiskeli ya walemavu iliyotolewa na Mke wa Mbunge wa
Mkuranga ajili ya watoto wenye uhitaji wa vifaa hivyo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Mkuranga Sharifa Nabalanganya akisoma risala ya Wilaya kwa Mgeni Rasmi.
Afande
Hamis, Msemaji wa dawati la Jinsia akiwaelezea Wazazi na Watoto kuwa
huru kuripoti unyanyasaji wowote unaofanywa kwa Watoto.
Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mkuranga akielezea Haki na wajibu wa Watoto.
Mdau Faidha Salum akifurahia jambo wakati wa Sherehe za Mtoto wa Afrika.
Wadau wa Haki za watoto wakifuatilia sherehe hizo
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiparang’anda wakisoma shairi Juu ya Watoto kulindwa ili wasome kwa amani na furaha.
Sehemu ya Wanafunzi wa shule hiyo.
Mke
wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akigawa zawadia kwa wanafunzi
wa shule ya Msingi Kiparang’ada wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto
wa Afrika,yaliyofanyika Juni 16 katika shule hiyo,wilayani Mkuranga.