UFARANSA, USWISI ZAPETA HATUA YA 16 KOMBE LA DUNIA, HONDURAS, ECUADOR HOI!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/ufaransa-uswisi-zapeta-hatua-ya-16.html
TIMU ya Taifa ya Ufaransa imefuzu
hatua ya 16 ya kombe la dunia kama washindi wa kwanza wa kundi E baada
ya usiku huu kuambulia pointi moja kufutia suluhu ya bila kufungana na
Ecuador.
Ufaransa wamefikisha pointi 7 kileleni
wakifuatiwa na Uswisi wenye pointi 6 katika nafasi ya pili baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Honduras.
Mabao yote ya Uswisi yamefungwa na Xherdan Shaqiri katika dakika ya 5, 30 na 70.
Kwa matokeo hayo, Ecuador waliomaliza
katika nafasi ya nne kwa pointi 4 na Honduras walioshika mkia bila
pointi yoyote wameaga rasmi mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia.
Wachezaji wa akiba: Banguera, Mendez, Rojas, Jaime Ayovi, Bagui, Saritama, Martinez, Gruezo, Bone.
Kadi ya njano: Erazo.
Kadi nyekundu: Antonio Valencia.
Kikosi cha Ufaransa: Lloris, Sagna, Koscielny, Sakho (Varane 61), Digne, Griezmann (Remy 79), Pogba, Schneiderlin, Matuidi (Giroud 67), Sissoko, Benzema.
Wachezaji wa akiba: Ruffier, Debuchy, Evra, Cabaye, Cabella, Valbuena, Mavuba, Mangala, Landreau.
Mwamuzi: Noumandiez Doue (Ivory Coast)
Kikosi cha Switzerland: Benaglio, Lichtsteiner, Inler, Xhaka, Behrami, Rodriguez, Mehmedi, Drmic, Djourou, Schaer, Shaqiri.