Taylor hataki kufungwa jela Uingereza
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/taylor-hataki-kufungwa-jela-uingereza.html
Rais wa zamani wa Liberia, ameanzisha harakati za kisheria kupinga amri ya kutumikia kifungo chake cha jela nchini Uingereza.
Taylor alifungwa jela kwa uhalifu dhidi ya
binadamu na anakataa kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa
ananyimwa haki ya kufurahia maisha yake.Mawakili wake wanasema kuwa kuzuiliwa kwake nchini Uingereza kunakiuka haki za binadamu kwa sababu ni mbali sana na yumbani kwa familia yake kuweza kusafiri huko kumuona.
Wanasema kuwa badala ya kutumikia kifungo Uingereza, aruhusiwe kutumikia kifungo hicho nchini Rwanda, pamoja na wafungwa wengine waliohukumiwa na mahakama maalum ya umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone.
Pia wanasema anahofia kushambuliwa na wafungwa wengine katika gereza la Frankland, Kaskazini mwa Uingereza.