Tanzania kubadili sheria kuhusu Shisha
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/tanzania-kubadili-sheria-kuhusu-shisha.html
Waziri wa afya nchini Tanzania,
amesema kuwa Tanzania inapanga kutathmini sheria ya sasa kuhusu matumizi
ya Sisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo matumizi ya
Shisha.
Dkt Seif Rashid Selemani amesema kuwa sheria
hiyo italenga kulinda afya ya watanzania hasa walio na uraibu wa Shisha
na pia kuhakikisha kuwa wanaotumia Shisha katika sehemu zengine duniani
wanapata kubadili mfumo wa maisha ili kulinda afya zao.Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija, umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana mjini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.
Lakini wataalamu wanaamini kuwa uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.
Madaktari walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wakisema kuwa waraibu wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani sawa na hatari inayowakabili wavutaji wa sigara.