TAARIFA KUHUSU MTOTO ALIYEZALIWA NA MKIA ANAYEABUDIWA KAMA MUNGU HUKO INDIA,
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/taarifa-kuhusu-mtoto-aliyezaliwa-na.html
Mvulana mdogo aliyezaliwa na
mkia unaofikia urefu wa inch saba anatarajia kufanyiwa upasuaji ili
utolewe licha ya kuwa anaabudiwa kama Mungu na watu wa jamii yake.
Arshid Ali Khan, mwenye miaka
13 anaweza kuathiriwa ukuaji wake kutokana na mkia huo ingawa unamfanya
aonekana kama alama ya uponyaji katika Jimbo la Punjab, India. Mtoto
huyo anayetumia kiti cha watu wenye ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu
wa jamii yake kama Mungu aliyepewa jina la Balaji.
Khan anasema mkia huo amepewa
na Mungu na anaabudiwa kwasababu ni Mungu huyo huyo ndiye anayemuomba
ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa kweli. Anasema hajisikii vizuri wala
vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona sawa tu. Arshid sasa anaishi na babu
yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake wawili baada ya baba yake kufariki
akiwa na umri wa miaka sita na mama yake kuolewa tena.
Source:Millardayo.com