Idadi ya wakimbizi yaongezeka duniani
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/idadi-ya-wakimbizi-yaongezeka-duniani.html
Shirika la kuwahudumia wakimbizi
la Umoja wa Mataifa UNHCR, linasema idadi ya watu waliopoteza makao yao
na kufanywa wakimbizi kutokana na vita ilizidi milioni hamsini mwaka
jana.
Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.Wengi wameishi katika kambi za wakimbizi kwa miaka mingi.
Vita nchini Syria, ni moja ya sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi hiyo ya wakimbizi, lakini pia kuna mizozo mingine katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchini Sudan Kusini ambayo imechangia idadi kubwa ya wakimbizi
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, linasema kuwa idadi hiyo ni ishara tosha ya athari za kukosa kuzuia mizozo. Pia limesema kuwa mataifa tajiri yanapaswa kufanya juhudi kuhifadhi wakimbizi hao.