Raia wa Costa Rica washerehekea ushindi
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/raia-wa-costa-rica-washerehekea-ushindi.html
Makumi ya maelfu wa raia wa
Costa Rica wamesherehekea ushindi wa timu yao ya taifa katika mechi za
kombe la dunia zinazoendelea nchini Brazil baada ya kuishinda italy kwa
bao moja kwa bila.
Raia hao waliokuwa wakipeperusha bendera
walisherehekea ushindi huo ambao umewaweka katika nafasi nzuri ya
kuingia katika awamu ya mchujo kwa mara piliUshindi huo pia unamaanisha kuwa Uingereza imebanduliwa nje ya mashindano hayo .
Wakati huohuo Ufaransa imepanda hadi katika nafasi ya kwanza ya kundi E baada ya kuicharaza Switzerland kwa mabao matano kwa mawili.
Katika mechi za kundi jengine Ecuador iliishinda Honduras kwa mabao mawili kwa moja katika mechi iliojaa msisimuko mkubwa.