MSF;Ugonjwa wa Ebola haudhibitiki tena
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/msfugonjwa-wa-ebola-haudhibitiki-tena.html
Afisa mwandamizi wa shirika la
madaktari wasio na Mipaka Medicine San Frontiers ameelezea kuwa
mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa matatu ya magharibi hauwezi
kudhibitika.
Mkurugenzi wa Oparesheni katika shirika hilo
Bart Janssens ameliambia shirika la habari la A.P kwamba ugonjwa huo
utasambaa hadi katika mataifa mengine iwapo hakutakuwa na mwitikio wa
kimataifa.Ugonjwa wa Ebola tayari umesababisha vifo vya takriban watu 330 nchini Guinea,Sierra leone na Liberia.
Bwana Janssens amesema kuwa shirika la MSF limefikia kikomo cha uwezo wake wa kukabiliana na ugonjwa huo.