POLISI AUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA UVAMIZI WA KITUO CHA POLISI KIMANZICHANA MKOANI PWANI
.!!!...TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA KUTISHA...!!!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/polisi-auawa-na-wengine-kujeruhiwa.html
.!!!...TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA KUTISHA...!!!
Mnamo 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana
Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema walivamia kituo
kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za
jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye
amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na
hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza
kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili
na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka
kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa
matibabu kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga.

Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo
bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam
alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana
mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA
MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo
Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
TAHADHARI; Vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA
PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na
silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za
haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio
hili. AMEN
