Kocha: Kaseja rudi Simba, unamkumbuka Maximo?
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kocha-kaseja-rudi-simba-unamkumbuka.html
- Kocha huyo alisema, kuna sababu tatu zinazomfanya Kaseja kuondoka Yanga kwani akibaki hatoweza kufanya kazi yake kwa furaha na mafanikio.
Kabla ya Yanga kumsainisha Barthez, Simba ilikuwa
imepiga hesabu za kumrudisha kipa wao huyo wa zamani ili apambane na Ivo
Mapunda ambaye hana mpinzani katika kikosi cha timu hiyo.
Kocha huyo alisema, kuna sababu tatu zinazomfanya
Kaseja kuondoka Yanga kwani akibaki hatoweza kufanya kazi yake kwa
furaha na mafanikio.
Alisema kwanza ushindani wa nafasi kati yake na
makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Barthez ni mkubwa. Pili anaonekana
hakubaliki kwa mashabiki wa Yanga na tatu ni ujio wa kocha Marcio Maximo
katika kikosi hicho.
Pazi alisema: “Mahali alipo Kaseja (Yanga),
kunaweza kumfanya astaafu kabla ya muda wake au hata kuendelea kucheza
soka kwa mashaka hivyo namtaka afikirie kurudi Simba ili kutunza heshima
na kufanya kazi yake kama ilivyokuwa awali.
“Kaseja si kipenzi cha mashabiki Yanga na
inapokuja wakati wa kazi anaweza kupata wakati mgumu kutokana na
kuzomewa na kumfanya kutojiamini akiwa kwenye kazi yake.
“Pia nimesikia Yanga wanamleta Maximo, nafikiri ni
hofu kwa Kaseja kwa sababu siku za nyuma kocha huyo alitofautiana naye
wakiwa Taifa Stars, aje Simba ili awe na amani.”
Pazi pia amemtaka kipa huyo kufuta ndoto za kustaafu soka wakati huu ili awe kocha akisema kipa huyo bado ana uwezo wa kucheza.
“Nafikiri wapenzi wa Simba wanatakiwa kumpa Kaseja
nafasi kwenye mioyo yao. Amefanya mengi na naamini akirudi ataweza
kufanya mengi na kumalizia soka lake Simba akiwa na heshima,”
alisisitiza.
