Mwanamuziki wa Bongo fleva, Linex ahoji mchango wa Sugu kwenye Muziki wa Tanzania: Ataka aone mifano ya Sugu ambayo ameifanya kwa wasanii wa kitanzania
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mwanamuziki-wa-bongo-fleva-linex-ahoji.html
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi ambaye ni mmoja wa wanamuziki wakongwe Tanzania hajamshawishi
Linex Sunday Mjeda ambaye amehoji mchango wake kwenye muziki.
Linex mjeda
Linex ameandika mtazamo wake
kupitia akaunti yake ya Facebook na Twitter, siku moja baada ya Sugu
kumtuhumu Zitto Kabwe kwa kile alichokiita ufisadi katika TANAPA na
NSSF kupitia kampuni ya Lekadutigite Ltd inayomilikiwa na wasanii wa Kigoma All Stars, akiwemo Linex.
“Hivi toka Sugu amekua mbunge
ni kitu gani alishawahi kuwafanyia wasanii wa Taifa hili, Tanzania na
akiwa kama waziri kivuli, amewahi kufanya nini kuinua kipato cha
wasanii? Je amejenga mazingira gani kuhakikisha wasanii hawawi ombaomba
wakutegemea misaada bali wajasiriamali?
"Eg. Amefikia wapi kwenye suala la hakimiliki na ufuatiliaji wake etc nimeuliza tu manaake kuna vitu vinaendelea sivielewi