Mtevu awakingia kifua mamalishe dhidi ya bomoabomoa Temeke
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mtevu-awakingia-kifua-mamalishe-dhidi.html
Mbunge
wa Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akitazama hali ilivyobaki baada ya
bomoabomoa iliyofanywa na Jiji kwenye vibanda vya mamalishe katika mtaa
wa Mbozi, Temeke.
BOMOA
Boboa ya vibanda vya mamalishe katika eneo la Viwanda la Mbozi, Temeke
Dar es Salaam, limezua mtafaruku kufuatia mbunge wa jimbo la Temeke,
Abbas Mtemvu kuwakingia kifua mamalishe hao.
Pamoja
na kuahidi kuchukua hatua ya kupambana kisheria na Halmashuri ya Jiji
la Dar es Salaam, inayoendesha bomoa boboa hiyo, Mtemvu amewata
mamalishe kuendelea na shughuli zao katika eneo hilo.
“Jambo
hili la kunyanyasa wananchi kwa kuwafukuza katika maeneo bila kufuata
taratibu halikubaliki hata kidogo. Sasa mimi nawasaka watu hawa wa
halimashauri ili kuzungumza nao, lakini wakati nafanyaa hivyo nawaagiza
muwendelee na shughuli zenu hapa, na atakayekuja kuwafukuza mwambieni
achukue kila kitu nami nitapambana naye kisheria”, Mtemvu amesema hayo
leo wakati akizungumza na baadhi ya mamalishe hao katoka eneo la viwanda
la Mbozi.
Mtemvu
alisema, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji hawakupaswa kuwafukuza mamalishe hao kwa kutumia
mgambo kuvunja vunja vifaa na kuondoka na baadhi ya vyakula kama ambavyo
imedaiwa, kwa sababu ujenzi wa barabara waliyopo hautarajiwi kufanywa
hivi karibuni.
Amesema
mbali na ujenzi wa barabara hiyo ambao Mtemvu alisema fedha za ujenzi
amezitafuta yeye kama mbunge, pia ilipaswa mamalishe hao kutengenezewa
mazingira mengine ya kuendelea na biashara zao kwa kuwa ni tengemeo kwa
wafanyakazi kwenye viwanda vinavyozunguka eneo hilo.
Mtemvu
alisema kutimuliwa bila kufanyiwa utaratibu mbadala, kutawafanya kinana
mama, wasichana na vijana wanaojishughulisha na biashara hiyo ya
mamalishe sasa kutafuta njia mbadala ya kuishi hata kama ni haramu jambo
ambalo litakuwa siyo jema kwa taifa.
Juzi,
Jiji kwa kutumia mgambo na tingatinga, walivamia eneo hilo la Mbozi na
kusambaratisha vibanda vyote vya mamalishe waliopungua 35, na inadaiwa
kwamba katika operesheni hiyo mgambo waliondoka na baadhi ya vyombo na
vyakula ambavyo hadi sasa havijulikani vilipo.
Mmoja
wa Mamalishe eneo la Mtaa wa Viwanda la Mbozi, Temeke Dar es Salaam,
Amina Saidi (kushoto) akilalamika mbele ya Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu, mbunge huyo alipotembelea eneo la tukio kuona hali halisi jana
mchana.