MASTAA WA BONGO MOVIE WANUSURIKA KATIKA AJALI YA GARI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mastaa-wa-bongo-movie-wanusurika-katika.html
Wasanii
nyota wa filamu ‘Bongo Movie’ wakiongozwa na mwenyekiti wao Steve
Nyerere wamenusurika katika ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo
jirani na Chalinze wakiwa njiani kuelekea Dar wakitokea mjini Dodoma
walipoenda kuhudhuria Tamasha la Uzalendo pamoja na Uzinduzi wa video ya
wimbo wa miaka 50 wikiendi iliyopita.
Chanzo
cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni kupasuka kwa matairi mawili ya gari
walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Brevis lenye nambari za usajili T
200 CRY hata hivyo Hakuna mtu aliyeripotiwa kufa wala kujeruhiwa. Vicent
Kigosi ‘Ray’, Shamsa Ford, Irene Uwoya, Johari na Jaccob Steven ‘JB’ ni
miongoni mwa wasanii waliokuwepo eneo la tukio.