Majeshi ya Iraq yapambana kwa ajili ya kituo cha mafuta.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/majeshi-ya-iraq-yapambana-kwa-ajili-ya_22.html
Majeshi ya Iraq na wanamgambo wa Sunni wanaopambana kugombania
udhibiti wa kituo kikuu cha kusafishia mafuta nchini humo waliendelea
na mapambano Alhamisi huko Beiji.
Mashahidi waliona moshi kutoka kiwandani huko na kusema bendera nyeusi ya Islamic state of Iran na Levant ilikuwa ikipepea kutoka kwenye jengo moja.
Maafisa wa usalama wa Iraq wanasema bado serikali ina udhibiti wa kituo hicho cha mafuta ambacho kipo nusu njia kati ya Baghdad na Mosul.
Marekani bado inaangalia jinsi ya kuwasaidia Iraq kupambana na wanamgambo ambao wamechukua udhibiti wa miji muhimu huko Kaskazini na kutishia mji mkuu.
Mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerali Martin Dempsey aliiambia kamati ndogo ya bunge Jumatano kwamba serikali ya Iraq imeomba msaada wa mashambulizi ya anga kutoka Marekani.
Amesema serikali inayoongozwa na washia ya Iraq imeshindwa kusaidia watu wake na kwamba viongozi wameshindwa kutimiza wajibu wao kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na wasunni na wakurdi.