Flatnews

Marekani yajiandaa kulinda maslahi yake Iraq


Meli ya Marekani USS George H.W. Bush.
Meli ya Marekani USS George H.W. Bush.

Marekani imeagiza kupelekwa kwa meli inayobeba ndege za kivita na silaha katika  ghuba ya uajemi, tayari kujibu mgogoro unaoendelea nchini Iraq.

Msemaji wa Pentagon  John Kirby amesema waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel  alitoa amri hiyo  Jumamosi kwa  meli hiyo kwa  jina USS George H.W. Bush  kupelekwa kwenye ghuba ya uajemi kaskazini.

Kirby anasema hatua hiyo ni muhimu na kwamba inawapa uwezo wana jeshi wa Marekani uwezo wa kuchukua hatua ikibidi  kulinda maisha ya wamarekani na maslahi yake nchini Iraq.

Wanamgambo wa kundi la Islamic State of Iraq and Levant katika siku za karibuni wamedhibiti maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo na wanaendelea kusogea kuelekea mji mkuu Baghdad.

Post a Comment

emo-but-icon

item