MAFIKIZOLO WAFUNGUKA KUHUSU DIAMOND PLATINUMZ...!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mafikizolo-wafunguka-kuhusu-diamond.html
Kwenye utoaji wa tuzo za MTV Africa Music Awards au MAMAs zilizofanyika 7 June jijini Durban, South Africa, Mafikizolo waliomba kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wao mpya ambao wamefanikiwa kuurekodi June 9 usiku kwenye studio za mkongwe Oskido kule JohannesburgBaada ya kurekodi hiyo kolabo, Theo wa Mafikizolo alisema: "Diamond ni mwepesi tofauti na nilivyotarajia, huyu ni miongoni mwa wasanii wa Africa tunaowataka, lengo letu ni kuufikisha muziki kwenye kila kona ya Afrika na ndio maana tumeomba kufanya kolabo na huyu staa wa Afrika Mashariki."
Kwenye sentensi ya mwisho ya exclusive interview na DStv.com, Theo amesema walimfahamu Diamond Platnumz kupitia kwa Davido, yaani walimuuliza Davido ni nani mkali wa Afrika Mashariki kwa sasa akawaambia Diamond.