LOWASSA KAMA KAWAIDA YAKE ATANGAZA MAAMUZI MAGUMU
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/lowassa-kama-kawaida-yake-atangaza.html
Waziri
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa ametangaza
kuanza kwa hatua za kuyarejesha kwenye Mamlaka za Serikali za Vijiji
mashamba 21 ya wawekezaji yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 10,000,
ambayo hayajaendelezwa.Akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Lomooti, Kata ya Lolkisale wilayani humo
alipokwenda kutembelea boma la kisasa la mfugaji Isaya Lembekure,
Lowassa alisema haiwezekani wananchi wa Monduli kukosa ardhi wakati,
kuna ardhi yao iliyohodhiwa na wachache bila kuendelezwa.“Monduli
tumechoka na uuzwaji wa ardhi. Kila mahali ni matatizo ya uuzwaji wa
ardhi. Sasa tunatangaza kuanza mchakato wa kuyarejesha mashamba yote ya
wawekezaji ambayo hayajaendelezwa. Tayari hatua mbalimbali zimeanza
kuchukuliwa ili kuyarejesha,” alisema Lowassa.Tamko
hilo la Lowassa, lilipokewa kwa shangwe na wananchi wa Wilaya ya
Monduli na limekuja wakati migogoro ya ardhi baina ya wawekezaji na
wananchi na wakulima na wafugaji imeshamiri nchini.Licha
ya kutoa agizo hilo, Lowassa ameendelea kukemea uuzajiwa wa ardhi
wilayani humo, unaofanywa kinyume cha taratibu na Serikali.Kuanzia
sasa kiongozi wa kijiji atakayebainika kuhusika kuuza ardhi kinyemela,
ang’olewe kupitia mikutano ya vijiji,” alisema Lowassa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib
Mbasha alisema tayari halmashauri hiyo imeanza maandalizi ya kuyarejesha
mashamba hayo kwa kuwataka wahusika wa mashamba hayo kujieleza kwa
nini hawajayaendeleza hadi leo.
“Halmashauri
inakusudia kuyafuta mashamba yote yasiyoendelezwa na yaliyotelekezwa,
hii ni kutokana na kushindwa kufuata masharti ya ardhi kama
ilivyoanishwa na sheria ya Ardhi namba 4,999 fungu la 44 na fungu la 48.
Nimetoa siku 90 watu hawa wajieleze,” alisema Mbasha.
Aliyataja
mashamba yanayotarajiwa kurejeshwa kwenye mamlaka za Serikali za Vijiji
kuwa ni Meru Enterprises namba 10, ACU LTD namba 2390, TANFORM LTD 47,
TANFORM 44 na Melembuki Kitesho Mollel namba 974 katika Kijiji cha
Lolkisale.
Mashamba
mengine ni The Monduli Parents Sec School, Musa Mamuya namba 2278 lipo
Makuyuni, David Pello 2275, Hillary Gadi namba 2474, Khalifan Said
Masoud 2276, Masoud Said Masoud 2277 yapo Kijiji cha Mswakini Juu.
Alitaja pia yaliyopo katika kijiji hicho ni ya Lucas Petro Kambei namba 2597 na Rungwa game Safari Ltd namba 2765.
Alisema
mashamba mengine ni Omary Daudi Mshana 1571, Saidi Rashid Lena namba
2549 yaliyopo Kijiji cha Naitolia, wakati mashamba mengine ni ya T.R
Msuya namba 3, Esimingori Estate Ranch namba 7/2, Saburi Estate Ltd
namba 7, Musa Y. Mamuya yaliyopo Makuyuni.