WABUNGE WAPENDEKEZA POSHO ZOTE ZA WABUNGE ZIKATWE KODI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/wabunge-wapendekeza-posho-zote-za.html
Wakichangia
mjadala wa mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa taifa na makadirio ya
mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2014/15, mbunge wa Ludewa Mhe
Deo Filikunjombe amesema wabunge wanapata mishahara, masurufu na posho
ambazo ni kubwa lakini hawalipi kodi huku mbunge Mhe. Lugola
akisisitiza mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa-brn- ni sehemu ya
michepuko inayokwamisha bajeti.
Aidha kwa
upande mwingine baadhi ya wabunge wamewataka wabunge kujitadhimini kama
wanalipa kodi za nyumba ili wawe mfano badala ya kuwasinikiza wananchi
kulipa kodi ya nyumba wakati wao hawalipi na kusisitiza sekta ya nyumba
nchni inaweza kuiiingizia serikali zaidi ya trilioni moja kwa mwaka.
Kwa
mujibu wa kalenda ya serikali inaonyesha zimebaki takribani siku kumi
kukamilika mwaka wa fedha wa serikali wa 2013/2014 ambapo baadhi ya
wabunge wameendelea kulalamikia kutokamilika kwa fedha za miradi ya
maendeleo iliyotajwa katika mwaka husika.