KUTOKA BRAZIL: Ronaldo kivutio, lakini Balotelli zaidi Brazil
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kutoka-brazil-ronaldo-kivutio-lakini.html

- Ndani ya ardhi ya Brazil kwa sasa kuna Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Robin van Persie, Arjen Robben, Diego Costa na wengineo, lakini ukizunguka katika mitaa ya Sao Paulo, Wabrazili wanavutika zaidi kumwangalia Balotelli. Wenyewe wanamwita ‘Maruku’ wakimaanisha kichaa.
Ndani ya ardhi ya Brazil kwa sasa kuna Cristiano
Ronaldo, Lionel Messi, Robin van Persie, Arjen Robben, Diego Costa na
wengineo, lakini ukizunguka katika mitaa ya Sao Paulo, Wabrazili
wanavutika zaidi kumwangalia Balotelli. Wenyewe wanamwita ‘Maruku’
wakimaanisha kichaa.
Popote ambapo kikosi cha Italia kinapoonyeshwa
katika televisheni watu wote waliopo katika baa mbalimbali za Sao Paolo
wanakaa kimya na kusikiliza kinachozungumzwa kuhusu Balotelli ambaye
ndiye anazungumziwa kwa muda mrefu na watangazaji.
“Tungependa kuwa na mchezaji kama yeye kikosini
kwetu Brazil. Anachangamsha timu. Unamkumbuka Edmundo? Alikuwa kama
yeye. Katika timu lazima uwe na mchezaji kichaa,” anasema dada mmoja
mhudumu wa baa ya Carcio de Italiano, Suzanne Almeda.
Mtu mmoja anajitokeza kumsifu Balotelli lakini
hapo hapo anatengeneza laana kwa Wataliano wasichukue ubingwa wa Kombe
la Dunia kwa sababu wakichukua wataifikia Brazil kwa idadi ya mataji
hayo.
Ikumbukwe kuwa katika fainali, Italia wamechukua
mara nne wakiifukuza Brazil ambayo imechukua mara tano. Wajerumani nao
wanaombewa dua mbaya na Wabrazili wa hapa kwa sababu wamechukua mara
tatu.
Cristiano Ronaldo anapendwa kwa sababu kubwa moja.
Anatoka katika nchi ambayo iliwatawala na kuwaachia lugha ya Kireno
ambayo ni Ureno. Kwa sababu Ronaldo anazungumza lugha wanayoielewa huku
kukiwa na Wareno wengi nchini Brazil, raia wa Brazil wanamuona kama
mwenzao.
Sijachunguza kwa umakini, lakini nadhani naweza
kuja na mjadala huu siku zijazo ukiendelea kusoma Mwanaspoti, nadhani
Messi atakuwa anachukiwa kwa sababu anatoka katika taifa lao pinzani,
Argentina.