Okwi ajisalimisha kwa Manji Dar
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/okwi-ajisalimisha-kwa-manji-dar.html
- Edgar Aggaba ambaye ni raia wa Uganda, atawasili nchini kesho Jumapili tayari kutatua mzozo baina ya straika huyo na Yanga ambao msimamo wa Manji ni kutaka Okwi akatwe sehemu ya Dola 40,000 za usajili anazodai au aongeze mkataba wa mwaka mmoja.
Edgar Aggaba ambaye ni raia wa Uganda, atawasili
nchini kesho Jumapili tayari kutatua mzozo baina ya straika huyo na
Yanga ambao msimamo wa Manji ni kutaka Okwi akatwe sehemu ya Dola 40,000
za usajili anazodai au aongeze mkataba wa mwaka mmoja.
Yanga wamefikia hatua hiyo kwa madai kuwa Okwi
waliyemnunua kwa dau la Dola 100,000 lakini anawasumbua na hajafanya
kazi katika miezi ya mwisho ya msimu uliopita kwa mujibu wa makubaliano.
“Nakuja Dar es Salaam wikiendi hii, naweza kuwa
huko Jumapili ili mchana nikutane na Mwenyekiti wa Yanga, hii ni klabu
kubwa hapa Afrika inaongozwa na viongozi makini ndiyo maana tulikubali
kuwauzia Okwi, tunataka kumaliza hili tatizo kwa kutumia mazungumzo bado
Okwi anataka kucheza Yanga,” alisema Aggaba.