KITOKOLOLO RAPA WA FM ACADEMIA AHAMIA BENDI YA MASHUJAA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kitokololo-rapa-wa-fm-academia-ahamia.html
Kitkololo akitangaza rasmi kujiunga na bendi ya Mashujaa leo kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Bw. Maximillian Luhanga.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Bendi ya Mashujaa Bw. Maximillian Luhanga akizungumza
katika mkutano huo wakati alipomtambulisha rapa Kitokololo kushoto
kutoka bendi ya FM Academia kulia ni King Dodoo mshauri wa bendi hiyo
na katikati.
…………………………………………………………………….
BENDI
ya Mashujaa imemchukua rapa, Kalidjo Kitokololo ‘Kuku’ kutoka bendi ya
FM Academia na kusaini naye Mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza kwenye ukumbi wa Milenium Business Park leo , Kijitonyama, Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi hiyo, Maximillian Luhanga amesema kupatikana kwa Chitokololo ni furaha kubwa kwao.

“Kalidjo
anakuwa rapa wa tatu katika bendi ya Mashujaa , baada ya Saulo John
maaurufu Ferguson na Sauti ya Radi, ambao wote ni wakali, kwa marapa
hao wote tunaamini bendi yetu itakuwa inatisha sana,”amesema Luhanga.
Maxmilian Luhanga amesema Kitokololo anaanza kazi mara moja baada ya kusaini mkataba mpya.
Kwa upande wake, Kitokololo mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema amekuja Tanzania kutafuta maisha na Mashujaa imempa ofa nzuri ndiyo maana amejiunga na bendi hiyo.
Amesema ameondoka vizuri FM Academia akiwa amewaaga vizuri wenzake ambao wameridhia kuondoka kwake.
Kitokololo amesema kwamba amejiunga na Mashujaa akimfuata King Dodo ambaye kimuziki ni baba yake , King Dodoo ndiye aliyemleta nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Mashujaa itamtambulisha rasmi mwanamuziki huyo katika onyesho maalum litakalofanyika ukumbi wa Letasi Lounge Ijumaa wiki hii.

Mashujaa
pia wanatarajiwa kuwa na ratiba ndefu mara baada ya mfungo mtukufu wa
ramadhani ambapo Maximillian Luhanga amewaambia mashabiki wa bendi hiyo
nchini kote kukaa mkao wa kula, Kwakuwa bendi hiyo itakuwa na ziara
karibu mikoa yote ya Tanzania ili kutoa burudani kwa mashabiki wao.