KIJANA AUAWA BAADA YA KUVAMIA NYUMBA NA KUMCHARANGA MAPANGA MWANAMKE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kijana-auawa-baada-ya-kuvamia-nyumba-na.html
Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30) ameuawa na wananchi
wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32) wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya Kalangalala mjini Geita .Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo inadaiwa kuwa watu watatu
akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao
na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.Baada ya Monica Lutonja kufungua walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu.
Hata
hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na kuanza
kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja na
wakaanza kumpiga hadi kumuua.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo
na kuongeza kuwa watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi
la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
